Kwa siku za nyuma, jumla ya idadi ya kondoo wanaofugwa hapa nchini
Tanzania ilikaribiana kuwa sawa na idadi ya mbuzi nchini kote. Kwa sasa,
idadi ya kondoo imepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na idadi ya
mbuzi. Hii imetokana na wafugaji kuhamishia mapenzi yao kwenye ufugaji
wa mbuzi.
Kama walivyo mbuzi, kondoo pia wanaweza kufugwa na wafugaji wadogo
wadogo na kwenye eneo dogo ambalo hutumika kwa kilimo pia. Kinachotakiwa
ni namna ya kuongeza mazao na kuwa na ufanisi. Kwa kuzingatia
yafuatayo, mfugaji wa kondoo ataweza kuwa na ufanisi mzuri.
Banda la kondoo
Banda na malazi ni lazima yawe mazuri na lenye nafasi ya kupitisha hewa
vizuri, linaloweza kuwakinga mifugo dhidi ya mvua, jua na upepo. Sakafu
iliyo nyanyuka ni nzuri zaidi.
Lakini sehemu ya mbele ya banda iwe na uwazi. Inashauriwa sakafu iwe na mwinuko kidogo.
Usafi
Ni lazima kinyesi kiondolewe kila siku ili kuweka banda katika hali ya
usafi na ukavu kila wakati. Hii, itasaidia kuzuia magonjwa ambayo
hushambulia kondoo mara kwa mara kama vile Pneumonia na kuoza kwato,
pamoja na kupunguza uwezekano wa kuwepo wadudu nyemelezi.
Kwa kondoo wanaochungwa wakati wa mchana, banda la kawaida lililoezekwa
linatosha kuwasitiri kondoo nyakati za usiku. Tenga walau skwea mita 1.5
kwa kila mnyama ili kuzuiuwezekano wa magonjwa yanayotokana na
msongamano.
Kwa kondoo wanaolishwa ndani, inatakiwa:
• Sehemu kavu, banda lenye hewa na kuezekwa vizuri (skwea mita 2)
• Kihondi kizuri cha kulishia ili kufanya malisho kuwa safi na kupunguza uharibifu.
• Sehemu nzuri ya nje inayowafaa kondoo kutembea. Tenga walau skwea mita
3 kwa kila kondoo. Kila mwanakondoo anahitaji eneo la kutosha kwa ajili
ya kukimbia na kucheza.
• Maji safi na jiwe la chumvi vinahitajika kuwepo wakati wote.
• Utahitajika kuwa na banda la ziada ama kwa muda kwa ajili ya kondoo
wenye mimba, kuzalia na kwa ajili ya wanakondoo. Pia, kwa kondoo
wanaoumwa.
• Banda la uzio kwa ajili ya kondoo unaweza kuwa rahisi zaidi kwa kuwa kondoo hawaruki wala kupanda juu.
Virutubisho kwa ajili ya kondoo
Kondoo hutumia muda mwingi wakati wa mchana kula majani na baadaye
hucheua na kutafuna. Wanapendelea zaidi kula majani na vichaka ambavyo
vina mchanganyiko wa madawa ya asili. Wanakondoo hujifunza kutoka kwa
mama zao ni nini chakula. Kama unawaanzishia aina mpya ya chakula, lisha
kwa kiasi kidogo na uweke kwenye sehemu walikozoea kulishiwa.
Kuwa makini na ukumbuke kuwa wanyama wanaopata lishe duni ni rahisi
kushambuliwa na magonjwa na hawana uwezo wa kukabiliana na vimelea vya
magonjwa. Kondoo jike asiyelishwa vizuri hawezi kubeba mimba. Uzalishaji
wa maziwa pia huwa kidogo kiasi cha kufanya watoto wake kuwa dhaifu na
kukua kwa shida.
Kuchunga
Kwa kawaida kondoo wanapenda kulisha kwa kula ardhini, lakini wanakula
aina tofauti za majani. Kondoo na ng’ombe wanakuwa na muunganiko na
kundi zuri la kujilisha kwa kula majani yaliyomo ardhini. Hii inatokana
na kuwa wanyama hawa hushambuliwa na wadudu na magonjwa tofauti na
hakuna anayedhuru mwingine. Kondoo hawaogopi mvua kama walivyo mbuzi,
lakini kusimama kwenye matope husababisha ugonjwa wa miguu na kuoza
kwato.
Ili kuepuka kulisha kupitiliza katika eneo moja, jambo linaloweza
kutengeneza na kusababisha vimelea, usiwaache kondoo wako kula sehemu
moja kwa muda mrefu zaidi ya wiki 2.
Kila kipande cha uwanda kinatakiwa kuachwa bila kulishiwa kondoo au
mbuzi kwa kipindi cha wiki sita. Unahitaji kuwa na walau vipande 4 vya
uwanda kwa ajili ya kuchungia kwa mzunguko. Hekari moja yenye malisho
mazuri, ni lazima itoe malisho ya kutosha walau kwa kondoo wanne na
watoto wao. Gawanya eneo unalohitaji kwa ajili ya kondoo wako mara nne
kisha ulishe kwa mzunguko katika eneo hilo.
Kwenye eneo lenye malisho duni unahitaji kuwapatia kondoo eneo kubwa
zaidi, na pengine kuwaongezea chakula chenye virutubisho. Tumia majani
ya malisho anayozidi wakati wa mvua kutengeneza hay kwa ajili ya
kulishia wakati wa kiangazi.
0 comments: