Dunia imejawa na makosa mengi, binadamu, wanyama,
bahari, ardhi na mimea kila sehemu unayoangalia, kuna makosa sehemu. Kama
unaweza kuyaangalia haya makosa kwa jicho la tatu ndipo unapoweza kufanikiwa
kama mjasiliamali na kushindwa kutambua haya makosa ni changamoto kubwa sana
kwa mjasiliamali.
Ujasiriamali unahusisha kutatua changamoto kubwa za
maisha za kila siku, kuanzia asubuhi tunapoamka mpaka jioni tunapopanda
kitandani. Hapa kati ya siku kuna milioni ya makosa ambayo yanasubiria utatuzi
na ufumbuzi lakini pia yanasubiria mjasiriamali mmoja ambaye atathubutu na
kuweza kubadilisha haya makosa kuwa chanzo cha pesa badala ya haya makosa kuwa
kilio kwake.
nimezaliwa katika familia maskini, familia ambayo
wazazi wanapambana kuweka mkate wa siku mezani, makosa makubwa ambayo
nimekutana nayo nikiwa mdogo ni ukkosefu wa taarifa, hili kosa kubwa saana
katika maisha. Kukosekana kwa taarifa kulifanya nishindwe kuwa kama vijana
wengine ambao walikuwa wanapata taarifa japo sidhani kama wengi wao walikuwa
wanajua jinsi ya kutumia hizo taarifa. Hii ikanipelekea kujiwekea lengo kuu la
kujipatia taarifa ya jambo moja kila siku. ( taarifa hizi si taarifa ya habari
) kwa kufanya hivyo ilibniwezesha kufahamu mambo mengi kuliko yale wenzangu
wanayoyapata.
inaendelea
0 comments: