MAANA YA UJASIRIAMALI
• Ujasiriamali ni hali ya kutumia mbinu mpya za kiubunifu na ujuzi katika utoaji wa huduma/ biashara.
• Ni hali ya kuweza kutambua fursa zilizokuzunguka ili kufikia ndoto zako kwa kutumia ubunifu
• Mjasiriamali ni mtu ambaye hutumia mbinu mpya na ubunifu , ujuzi na maarifa katika utoaji wa huduma
• Mjasiriamali
ni mtu anayetaka mabadiliko katika maisha kutoka hapo alipo na
kuboresha maisha akiwa na ujasiri wa kufikia malengo yake kwa kuthubutu.
• SIFA ZA MJASIRIAMALI
• àNi mbunifu
• àNi mdadisi wa mambo
• àAnashauhuku ya kujifunza
• kutoka kwa waliofanikiwa
• àNi mvumbuzi katika utendaji
• àAnathubutu katika kufanya
• mambo(Sio mwoga).
JINSI YA KUBUNI WAZO ENDELEVU LA BIASHARA
• Wazo
la biashara ni maelezo mafupi yahusuyo biashara au shughuli unayotaka
kufanya.Kwa mfano kushona nguo,kulima bustani, kufuga kuku, kuuza
chakula cha mifugo n.k.
• Wazo la biashara linahusu:
n Nini unachotaka kufanya kumridhisha
mteja/kukidhi kiu yake.
nNi huduma gani/bidhaa unayotaka kuuza
sokoni.
nWateja wako ni wa aina gani?
nJinsi ya kutoa huduma/biashara yako
UMAFUTI (SWOT ANALYSIS)
Ni kifupisho katika uchambuzi wa wazo endelevu la biashara.
U- Uwezo Ni pamoja na kuwa na ujuzi, uzoefu na maarifa kwa biashara
unayotaka kuifanya/kuwa na uwezo wa kutoa huduma /biashara unayotaka
kuifanya.
MA- madhaifu
• Upungufu ulionao ambao unaweza kuwa changamoto kwa biashara unayotaka kuifanya
• Kwa mfano mtaji mdogo, kodi ya pango iko juu.
FU-fursa
• Hali
na mazingira rafiki kwa biashara /huduma unayotaka kuitoa. Kwa mfano
hakuna mtu anayetoa huduma kama unayotaka kuitoa, bei ni rahisi kwa
walio wengi, sehemu ya biashara ina muingiliano wa watu mbalimbali
T- tishio
• Vizingiti katika ufanyaji biasha unayotaka kuifanya, kwa mfano uwezekano wa watu wengi kufungua biashara kama ya kwako, kubadilika kwa hali ya hewa n.k.
JINSI YA KUTANGAZA BIASHARA YAKO
• Kutangaza
biashara /huduma yako ni mbinu unazotumia kuhakikisha unavutia wateja .
Ni jinsi ya kukidhi kiu ya wateja kwa kuwapa huduma nzuri zaidi ya watu
wengine wanaotoa huduma kama ya kwako.
• Mjasiriamali hutumia maarifa, ujuzi na ubunifu ili kuwafanya wateja waende kwake
• Kabla
haujaandaa mpango wa masoko kama mjasiriamali ni vyema kufanya utafiti
kuhusu huduma unayotaka kuitoa ili uweze kutambua mapungufu na
changamoto walizonazo wengine ili uje na maarifa na mbinu mpya zakuweza kuwavutia wateja wengi zaidi.
VITU 4 VYA KUZINGATIA KATIKA MASOKO (BBMK
• B-Bidhaa ya aina gani unataka kuiweka sokoni na ina utofauti gani na bidhaa za wengine.
• B-Bei ya bidhaa unayotaka kuiweka sokoni. Katika kupanga bei lazima ujue washindani wako wana gharama gani.
• Kama
gharama ziko juu au chini na je, wateja wataweza kumudu, na kama
gharama iko juu bidhaa yako umeiongezea ubora gani ili wateja waje kwako
na si kwa mwingine.
• M- Mahali unapotaka kuweka biashara yako
• Uchaguzi mzuri wa eneo la kufanyia shughuli zako ni muhimu kwani ni rahisi kufikiwa na wateja wengi.
• Kama biashara yako haipo karibu na wateja lazima utafute mbinu za kuweza kuwafikia wateja wako ili waweze kuridhika na kufurahia huduma yako.
• K-Kutangaza bidhaa: Kama
mjasiriamali lazima uwe na mbinu mahususi jinsi utakavyofanya
bidhaa/huduma yako ijulikane na kuvutia wengi zaidi.Kutangaza ni
kuifanya bidhaa yako/huduma iweze kujulikana na mbinu unazozitumia ili
mteja aendelee kununua bidhaa/ huduma yako.
GHARAMA ZA UENDESHAJI KATIKA UTOAJI HUDUMA
• Katika uendeshaji wa biashara kuna gharama za aina mbili ambazo ni:
• Gharama za moja kwa moja; Hizi ni gharama unazotumia kununua bidhaa unayotaka kuuza
• Kama vile, mali gafi, nguvu kazi n.k.
• Gharama ambazo si za moja kwa moja: Hizi ni gharama nyingine zinazojitokeza wakati wa uendeshaji wa biashara yako, kwa mfano;umeme,ukarabati, bima, riba kwenye mikopo, pango n.k
KUTUNZA KUMBUKUMBU
• Ni muhimu kutunza kumbukumbu katika biashara
• Kutunza kumbukumbu husaidia katika kukokotoa faida au hasara iliyopatikana katika biashara.
• Hutoa takwimu kuhusu mwelekeo wa biashara na huongeza ufanisi katika usimamizi wa biashara.
• Wakati wa kulipa kodi utunzaji wa kumbukumbu husaidia kulipa kiwango kinachostahili.
• Kushindwa kutunza kumbukumbu kunaweza kusababisha kulipa
kodi chini ya kiwango kinachohitajika (underpay) au huweza kupunjwa kwa
kulipa kodi kubwa zaidi ya kiwango kinachohitajika.(Overpay).
• Kumbukumbu za fedha katika biashara ni muhimu katika mpango wa mauzo na gharama pamoja na mtiririko wa fedha zinazoingia na zinazotoka (Cash in and Cash out)
• KUMBUKUMBU ZA MAUZO NA GHARAMA
• Hizi ni kumbukumbu ambazo huonyesha mauzo, gharama zilizotumika na faida iliyopatikana
• Ni vizuri kuwa na kumbukumbu za kila siku, wiki, mwezi na mwaka mzima
• Msingi wa hizi kumbukumbu ni kuwa na mpango wa mauzo na gharama ili kuwa rahisi kufanya tathimini ya maendeleo ya biashara
• Faida kutoka kwenye mauzo tunaipata kwa kuchukua jumla ya mauzo na kutoa gharama zote zilizotumika
• Kwa mfano kama umeuza 50,000, kibarua ukamlipa 2000, ushuru3000, bidhaa uliyouza uliinunua 20,000
• Faida=50,000 - (2000 +3000+20,000)
• Faida=50,000 -25,000= 25,000
MPANGO WA MTIRIRIKO WA FEDHA
• Huu ni mtiririko ambao huonyesha kiasi cha fedha zinazoingia na kutoka katika biashara yako.
• Fedha zinaweza kutoka kwa mfano katika ununuzi wa malighafi, kulipa mkopo, kununua vifaa n.k.
• Fedha zinazotoka husaidia katika kutengeneza faida baadae
• Mtiririko wa fedha huonyesha
1.Fedha zinazoingia
a. Kiwango cha fedha mwanzoni
mwa mwezi
b.Fedha zilizoingia kutokana na mauzo
c. Fedha zinazoingia kutoka vyanzo vingine
JUMLA YA FEDHA ZILIZOINGIA =
2.Fedha zinazotoka
a.Kwa kununua malighafi na vifaa vingine
b. Kwa ajili ya nguvu kazi
c. Gharama zisizo za moja kwa moja
d.Kulipia mkopo(marejesho)
e. Gharama nyingine
• JUMLA YA FEDHA ZILIZOTOKA =
KIWANGO CHA FEDHA MWISHO WA MWEZI
• Kukokotoa kiwango cha fedha Ulichonacho(baki) =fedha iliyoingia kutoa fedha iliyotoka
• Kiwango cha fedha kilichobaki mwishoni mwa mwezi ndio kianzio kwa mwezi unaoanza
0 comments: