Vyombo vya habari vyabanwa lugha za alama
Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu, Dk Abdallah Possi akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana kuhusu kutoa usawa wa habari kwa watu wenye ulemavu. Mwingine ni msaidizi wake, Severine Kapinga.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Dk Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuanza mara moja kutumia lugha za alama, tafsiri na majina sahihi ya makundi ya watu wenye ulemavu ili kuondoa dhana ya unyanyasaji na kutoa haki sawa ya kupata habari kwa kundi hilo.
Pia alivihimiza vyombo hivyo kuanza kupigania sasa haki za walemavu kama vilivyo mstari wa mbele kupigania haki za makundi mengine yakiwemo ya jinsia ili na kundi hilo nalo lipate haki sawa katika jamii.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Possi alisema agizo hilo linapaswa kutekelezwa mara moja kwa kuwa lipo tayari katika Sheria Namba Tisa ya Mwaka 2010 ya Watu Wenye Ulemavu.
“Tunadhani vyombo vya habari ni silaha muhimu katika kuleta mabadiliko, ndio maana tunavitaka vyenyewe vianze kuyahimiza mabadiliko yatakayowatambua walemavu kama watu wenye haki sawa na wengine. Tunataka kuanzia sasa suala hili lipewe kipaumbele kama ajenda nyingine kama vile jinsia zilivyopewa kipaumbele katika vyombo hivi,” alisisitiza Dk Possi.
Alivitaka vyombo hivyo hasa magazeti, televisheni na redio kutumia majina sahihi ya ulemavu na kuachana na majina yanayoashiria unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu.
“Vyombo vingi kwa sasa vinatumia majina kama vile vilema, albino, kipofu au kiziwi, haya majina kiukweli yanaashiria unyanyapaa kwa watu hawa, naviomba vyombo hivi viende kwenye taasisi sahihi kama vile Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) ili kupata namna nzuri ya kutumia majina ya makundi hayo,” alisisitiza.
Alitoa mfano wa majina sahihi yanayopaswa kutumiwa na vyombo hivyo kwa watu wasioona kuwa ni watu wenye uoni hafifu, viziwi ni wanaotumia lugha ya alama na watu wenye ualbino badala ya walemavu wa ngozi.
About author: FASHION NEWS TANZANIA
Cress arugula peanut tigernut wattle seed kombu parsnip. Lotus root mung bean arugula tigernut horseradish endive yarrow gourd. Radicchio cress avocado garlic quandong collard greens.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: