Misingi Mitano(5) Muhimu Ya Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali na Biashara.
by
FASHION NEWS TANZANIA
7:41:00 AM
Katika ulimwengu
wa sasa ambao ajira zimekuwa ngumu na shida kupatikana, ujasiriamali na
biashara vimekuwa ndio kimbilio la wengi. Watu wengi wanaingia kwenye
biashara kama njia kuu ya kujipatia kipato.
Pamoja na biashara kuonekana kuwa
kimbilio la wengi sio wote wanaoingia kwenye biashara wanafanikiwa.
Tafiti zinaonesha kwamba asilimia tisini ya biashara zinazoanzishwa
zinakufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Na hata hizo zinazovuka mwaka
mmoja asilimia tisini hufa baada ya miaka mitano. Hivyo kama mwaka huu
zimeazishwa biashara mia moja basi miaka mitano ijayo ni biashara moja
tu itakayokuwa bado inadumu.
Kwa nini biashara nyingi zinashindwa kudumu?
Biashara nyingi zinakufa kutokana na
ukosefu wa elimu muhimu kuhusiana na biashara na ujasiriamali. Watu
wengi wanaoingia kwenye biashara wanaingia kwa kuangalia tu ni kitu gani
watu wengine wanafanya na wao kufanya hivyo hivyo.
Biashara ni rahisi sana kufanya ila
ni ngumu kuendesha na kuikuza mpaka iweze kukupa faida kubwa sana. Ili
uweze kuendesha na kukuza biashara itakayokupa faida kubwa ni muhimu
kuchukua muda na kujifunza vitu vya muhimu vinavyohusiana na biashara.
Leo tutajifunza misingi mitano muhimu
ya biashara ambayo kila biashara inatakiwa kuizingatia. Wewe kama
mjasiriamali una jukumu la kujifunza na kufuata misingi hii ili uweze
kufikia malengo yako kwenye ujasiriamali na biashara.
Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.
- Kutengeneza thamani.
Ili biashara iweze kukua na
kutengeneza faida ni lazima itengeneze bidhaa au huduma ambayo ni ya
thamani kwa wateja. Ni lazima utoe bidhaa au huduma ambayo watu
wanaihitaji sana ili kuboresha maisha yao. Kama hujaanza biashara
fikiria ni kitu gani cha thamani ambacho watu wanakihitaji ila
wanakikosa, kisha anza kuwapatia na utajenga biashara kubwa. Kama tayari
unafanya biashara angalia ni kitu gani cha thamani unachotoa kwa watu
na angalia jinsi unavyoweza kuboresha ili kupata wateja wengi zaidi.
- Soko.
Kuwa na kitu chenye thamani pekee
bado haikutoshi kutengeneza biashara kubwa, ni lazima kuwe na soko
linalohitaji bidhaa au huduma hiyo. Hata kama soko lipo bado sio rahisi
kwa kila mtu kujua kwamba unatoa huduma muhimu. Hivyo ni muhimu kutafuta
soko la biashara yako kwa njia mbalimbali zikiwemo matangazo. Inakubidi
uhakikishe watu wanajua uwepo wa biashara yako na utengeneze uteja ili
watu waje kupata thamani unayotoa. Kukosa soko la uhakika ni chanzo cha
kufa kwa biashara nyingi.
- Kuuza.
Ili biashara ikue ni lazima uweze
kuuza thamani uliyotengeneza. Ni muhimu uweze kuwashawishi watu wanunue
bidhaa au huduma unayotoa. Kuuza ndio moyo wa biashara ambapo kama
usipokuwa makini ni rahisi kwa biashara kufa.
- Kufikisha thamani.
Kama umewaahidi wateja wako kwamba
bidhaa ama huduma unayotoa itaboresha maisha yao basi hakikisha hicho
ndio kitu kitakachotokea kwa wateja. Ni lazima uweze kufikisha thamani
uliyoahidi kwa wateja. Kwa kushindwa kufanya hivi wateja watakuona wewe
ni tapeli na hawatanunua tena bidhaa yako. Kama biashara itashindwa
kutengeneza wateja wanaojirudia ni lazima itakufa.
- Fedha.
Usimamizi wa fedha ni muhimu sana
kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza
mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha
fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana
na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara
nyingi.
Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa
biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya
mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu
kuzingatia misingi hiyo.
Kwa ushauri na muongozo wa biahsara, piga simu 0713 666 445.
PENDA BIASHARA, JIFUNZE BIASHARA.
Cress arugula peanut tigernut wattle seed kombu parsnip. Lotus root mung bean arugula tigernut horseradish endive yarrow gourd. Radicchio cress avocado garlic quandong collard greens.
0 comments: