NINI TOFAUTI KATI YA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA?

Nimekuwa nikijiuliza nini tofauti kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara?



Mara kadhaa maneno haya yamekuwa yakitumika sehemu tofauti tofauti na kupelekea wengi kufikiri kuwa yana maana sawa, lakini ukweli ni kwamba yana maana tofauti. Wote hawa wanamiliki biashara lakini wanatofautina katika mambo mbalimbali yahusuyo biashara zao.

Mfanyabishara ni mtu ambae anaanzisha shughuli za biashara kutokana na fursa iliyopo kwenye soko ambalo analihudumia. Mara nyingi wazo la biashara hizi linatokana na kuona biashara nyingine inayofanya vizuri sokoni. Mfanyabishara huweza kubadili mambo madogo madogo ili kuboresha biashara yake kwa kuangalia mapungufu ya chanzo cha wazo lake sio lazima yawe ya kibunifu.




Wakati Mjasiriamali yeye hutumia ubunifu kuanzisha biashara na hufanya juu chini kuhakikisha kuwa wazo lake limetimilika. Hutambua soko lake na kutengeneza bidhaa au huduma ya kipekee amabayo itaweza kukidhi mahitaji ya soko / wateja wake. Ni mbunifu na hupendelea kuona ameanzisha jambo jipya na linakuwa.

Ujasiriamali ni mgumu ukilinganisha na ufanyabishara, lakini matunda yake ni mazuri. Ukiwa mjasiriamali ni rahisi sana kuwa na uhuru wa kiuchumi na kifedha ukilinganisha na mfanyabishara. Biashara ya mjasirimali hukua na kuimarika kipindi kinavyosogea.

Je wewe ni mjasiriamali au mfanyabishara? Je unafanya tu biashara au upo katika kiwango cha kuitwa mjasiriamali?

0 comments: