Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko
lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia,
linaweza kutumika kama malisho ya mifugo
Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha
mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa
kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa
ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa
sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka.
Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa
baada ya kufunga na kukomaa vizuri.
Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika
ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini
(20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).
Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.
Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.
Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.
Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa
zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu
wowote kulingana na matakwa ya mkulima. Mbolea za samadi na zenye asili
ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za
mbegu huhitajika kwa hekta moja. Katika upandaji kwenye kitalu ni
vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari
uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika
mbegu.
Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika
kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche. Hii itasaidia kuwa na
miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili
kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta.
Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo
kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate
mshtuko wa uhamishaji shambani.
Kuhamisha na kupanda
Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati
huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha
sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo
ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na
ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na
unyevu wakati wote.
Nafasi kati ya mmea
Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea
hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati
ya mstari na mstari.
Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.
Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima
akawa mwangalifu ili asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga
hufunika ardhi, hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu
hakuna haja ya kupalilia.
Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta moja hutoa mavuno kiasi chatani 50-80.
Aina za kabichi
Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo:
** Majina hayo yanabaki kama yalivyo kutokana na sheria za hati miliki ya watafiti.
0 comments: