HUAWEI yaahidi kutoa motisha

HUAWEI yaahidi kutoa motisha kwa wasambazaji wao nchini Tanzania



Hivi karibuni Kampuni ya Huawei Device Tanzania ilifanya mkutano wake wa kwanza wa wasambazaji wa simu za mkononi wakitilia mkazo katika mipango ya ukuaji kwa kampuni ya Huawei Device Tanzania na wadau wao waliopo mikoani katika soko la Tanzania kwa ujumla. Mkutano huu uliyofanyika tarehe 30 Mwezi Aprili katika Hoteli ya Double tree jijini Dar es Salaam, ulisherekea juhudi na msimamo wa muda mrefu wa wauzaji wa simu za mkononi Huawei Device Tanzania.

Wauzaji waliothibitika wa simu za Huawei nchini kote walikaribishwa. Wauzaji  waliungana na timu ya Huawei Device Tanzania kutoka mikoa yote mikuu kama, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, Dodoma, Tanga, Morogoro, Singida, Kagera, Kigoma na Bukoba.

Katika mkutano huo, Huawei Device Tanzania waliweka msisitizo katika haja ya kusaidia ukuaji kwa kutoa motisha kubwa. Bwana Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania alitangaza kuwa 10% ya mapato ya Huawei Device Tanzania yatatengwa kama uwekezaji wa kimasoko ili kuongeza na kuboresha bidhaa za Huawei.



Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania akitoa hotuba katika mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Akiongea katika mkutano huo, Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania alisema “tunafuraha kuweza kuzungumza na wadau wetu ambao watatuwezesha kuwa wauzaji wa simu za mkononi bora na namba Moja nchini Tanzania, kutoka nafasi ya Pili ambapo tuna % 22 ya hisa katika soko” (Q1, 2016).

Pia kutoa motisha Zaidi, Huawei walitangaza mpango mahususi ambapo wauzaji wakuu watazawadiwa dola za kimarekani 20,000 kwa mshindi wa kwanza  na nafasi ya pili atapewa dola za kimarekani 10,000.

Bwana Wang aliwapongeza Zaidi wauzaji kwa kusaidia Huawei Device Tanzania na Zaidi ya wauzaji 50 walipewa vyeti kuthibitisha kuwa wanauza simu halisi na orijino  za Huawei.



Timu ya Huawei Device Tanzania katika picha ya pamoja na wauzaji wa simu za Huawei  nchini Tanzania waliohudhuria mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.

Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania pia aliwapongeza wasambazaji na wauzaji wa rejareja waliokuwepo kwa ufanyaji kazi wao mzuri, na msaada endelevu na tumaini kwa biashara nzuri Zaidi mwaka ujao.

Wauzaji walishukuru juhudi za Hauwei katika kuboresha kiwango cha ubora cha simu na walikiri ubora wa hali ya juu ya simu za Huawei zenye marejesho ya % 0.02. Pia walitilia mkazo msimamo wa Huawei katika kutoa simu bora na kuungana mkono na kampeni ya TCRA kuondoa simu zisizo halisi nchini Tanzania.

Katika mkutano huo Huawei Device Tanzania walitangaza simu mpya ambazo zitakua sokoni hivi punde kama P9, Mate 8, GR5, GR3, Y6 Pro, Y3 II na Y3 Lite kuhakikisha wateja wote wa Tanzania wana uwanja mpana wa uchaguzi.



Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania (kushoto) akiwapatia vyeti wauzaji wa simu za Huawei Salum Otonde na Mkewe kuthibitisha kuwa wanauza vifaa vilivyo halisi na bora, katika mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania.



Bw. Wang Guang Jun, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Device Tanzania akimpatia cheti muuzaji wa simu za  Huawei, Tito Mahenge kuthibitisha kuwa anauza simu zilizo halisi na bora; Wakati wa mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Bwana Hu Xiangyang Jacko, Meneja wa Huawei Device nchini Tanzania.



Wauzaji kadhaa wa vifaa vya Huawei Tanzania wakitembelea Baadhi ya sehemu za maonyesho ya simu mpya za Huawei, katika mkutano  na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.



Baadhi ya zawadi mbalimbali zilizogawiwa kwa wauzaji wa simu za Huawei waliohudhuria mkutano mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii.



Mmoja wa wauzaji wa vifaa vya Huawei akiweka sahihi katika ukuta wa wageni wa Huawei katika mkutano mkutano na wauzaji wa simu za Huawei ujulikanao kama Huawei Device Tanzania Dealer Congress 2016 uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii

0 comments: