Fuga kondoo kisasa uboreshe pato lako


Kwa siku za nyuma, jumla ya idadi ya kondoo wanaofugwa hapa nchini Tanzania ilikaribiana kuwa sawa na idadi ya mbuzi nchini kote. Kwa sasa, idadi ya kondoo imepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na idadi ya mbuzi. Hii imetokana na wafugaji kuhamishia mapenzi yao kwenye ufugaji wa mbuzi.

Kama walivyo mbuzi, kondoo pia wanaweza kufugwa na wafugaji wadogo wadogo na kwenye eneo dogo ambalo hutumika kwa kilimo pia. Kinachotakiwa ni namna ya kuongeza mazao na kuwa na ufanisi. Kwa kuzingatia yafuatayo, mfugaji wa kondoo ataweza kuwa na ufanisi mzuri.
Kondoo hupenda kujilisha kwenye makundi
Kondoo hupenda kujilisha kwenye makundi

Banda la kondoo
Banda na malazi ni lazima yawe mazuri na lenye nafasi ya kupitisha hewa vizuri, linaloweza kuwakinga mifugo dhidi ya mvua, jua na upepo. Sakafu iliyo nyanyuka ni nzuri zaidi.
Lakini sehemu ya mbele ya banda iwe na uwazi. Inashauriwa sakafu iwe na mwinuko kidogo.

Usafi
Ni lazima kinyesi kiondolewe kila siku ili kuweka banda katika hali ya usafi na ukavu kila wakati. Hii, itasaidia kuzuia magonjwa ambayo hushambulia kondoo mara kwa mara kama vile Pneumonia na kuoza kwato, pamoja na kupunguza uwezekano wa kuwepo wadudu nyemelezi.
Kwa kondoo wanaochungwa wakati wa mchana, banda la kawaida lililoezekwa linatosha kuwasitiri kondoo nyakati za usiku. Tenga walau skwea mita 1.5 kwa kila mnyama ili kuzuiuwezekano wa magonjwa yanayotokana na msongamano.

Kwa kondoo wanaolishwa ndani, inatakiwa:
• Sehemu kavu, banda lenye hewa na kuezekwa vizuri (skwea mita 2)
• Kihondi kizuri cha kulishia ili kufanya malisho kuwa safi na kupunguza uharibifu.
• Sehemu nzuri ya nje inayowafaa kondoo kutembea. Tenga walau skwea mita 3 kwa kila kondoo. Kila mwanakondoo anahitaji eneo la kutosha kwa ajili ya kukimbia na kucheza.
• Maji safi na jiwe la chumvi vinahitajika kuwepo wakati wote.
• Utahitajika kuwa na banda la ziada ama kwa muda kwa ajili ya kondoo wenye mimba, kuzalia na kwa ajili ya wanakondoo. Pia, kwa kondoo wanaoumwa.
• Banda la uzio kwa ajili ya kondoo unaweza kuwa rahisi zaidi kwa kuwa kondoo hawaruki wala kupanda juu.

Virutubisho kwa ajili ya kondoo
Kondoo hutumia muda mwingi wakati wa mchana kula majani na baadaye hucheua na kutafuna. Wanapendelea zaidi kula majani na vichaka ambavyo vina mchanganyiko wa madawa ya asili. Wanakondoo hujifunza kutoka kwa mama zao ni nini chakula. Kama unawaanzishia aina mpya ya chakula, lisha kwa kiasi kidogo na uweke kwenye sehemu walikozoea kulishiwa.
Kuwa makini na ukumbuke kuwa wanyama wanaopata lishe duni ni rahisi kushambuliwa na magonjwa na hawana uwezo wa kukabiliana na vimelea vya magonjwa. Kondoo jike asiyelishwa vizuri hawezi kubeba mimba. Uzalishaji wa maziwa pia huwa kidogo kiasi cha kufanya watoto wake kuwa dhaifu na kukua kwa shida.

Kuchunga
Kwa kawaida kondoo wanapenda kulisha kwa kula ardhini, lakini wanakula aina tofauti za majani. Kondoo na ng’ombe wanakuwa na muunganiko na kundi zuri la kujilisha kwa kula majani yaliyomo ardhini. Hii inatokana na kuwa wanyama hawa hushambuliwa na wadudu na magonjwa tofauti na hakuna anayedhuru mwingine. Kondoo hawaogopi mvua kama walivyo mbuzi, lakini kusimama kwenye matope husababisha ugonjwa wa miguu na kuoza kwato.

Ili kuepuka kulisha kupitiliza katika eneo moja, jambo linaloweza kutengeneza na kusababisha vimelea, usiwaache kondoo wako kula sehemu moja kwa muda mrefu zaidi ya wiki 2.

Kila kipande cha uwanda kinatakiwa kuachwa bila kulishiwa kondoo au mbuzi kwa kipindi cha wiki sita. Unahitaji kuwa na walau vipande 4 vya uwanda kwa ajili ya kuchungia kwa mzunguko. Hekari moja yenye malisho mazuri, ni lazima itoe malisho ya kutosha walau kwa kondoo wanne na watoto wao. Gawanya eneo unalohitaji kwa ajili ya kondoo wako mara nne kisha ulishe kwa mzunguko katika eneo hilo.

Kwenye eneo lenye malisho duni unahitaji kuwapatia kondoo eneo kubwa zaidi, na pengine kuwaongezea chakula chenye virutubisho. Tumia majani ya malisho anayozidi wakati wa mvua kutengeneza hay kwa ajili ya kulishia wakati wa kiangazi.

Kabichi, faida lukuki kiuchumi na kiafya


Unaweza kulima kabichi msimu wote wa mwaka. Soko lake ni la uhakika katika kipindi chote na ni muhimu kwa afya. Pia, linaweza kutumika kama malisho ya mifugo

Kabichi ni moja ya mazao yaliyomo katika jamii ya mimea inayojumuisha mimea ya kaulifulawa (cauliflower ), kabichi ya kichina na kale. Kwa kawaida kabichi hupandwa kwa msimu mmoja, lakini iwapo itakuzwa kwa ajili ya kutoa mbegu hukuzwa zaidi ya msimu mmoja. Endapo inalimwa sehemu yenye maji ya kutosha, inaweza kulimwa msimu wote wa mwaka. Kichwa cha kabichi kinapofunga vizuri, hutumika kama chakula na huvunwa baada ya kufunga na kukomaa vizuri.

Mizizi: Mizizi ya kabichi hutawanyika ardhini vizuri. Kwa kawaida, huenda chini kiasi cha sentimita ishirini (20 sm), na hujitawanya kwa kiasi cha sentimita sabini na tano (75sm).

Shina: Shina la mmea wa kabichi huwa na rangi ya kijani au zambarau. Hii hutegemeana na aina ya kabichi, na kwa kawaida ni fupi.

Hali ya hewa: Kabichi hustawi vyema katika sehemu yenye hali ya baridi, hali ya joto jingi haifai kwa kabichi kwa kuwa huathiri uotaji na ukuaji wake. Joto jingi pia husababisha kulegea kwa vichwa vilivyofunga. Zao hili hustawi vema katika maeneo yenye mwinuko wa zaidi ya mita 100 toka usawa wa bahari.

Udongo: Zao hili linaweza kustawishwa kwenye udongo wa aina yoyote mradi tu udongo huo usiwe na chumvichumvi nyingi na usiotuhamisha maji. Udongo wa kichanga na ule usio na rutuba ya kutosha husababisha kabichi kukomaa upesi na kuzaa kabichi hafifu zenye vichwa vidogo.

Kitalu: Kitalu ni muhimu katika uzalishji wa zao hili. Ni vema kutengeneza matuta yenye upana wa mita moja, na urefu wowote kulingana na matakwa ya mkulima. Mbolea za samadi na zenye asili ya chokaa zichanganywe vizuri kwenye udongo. Kiasi cha gramu 500 za mbegu huhitajika kwa hekta moja.  Katika upandaji kwenye kitalu ni vizuri kutengeneza mistari katika tuta, umbali toka mstari hadi mstari uwe sentimita ishirini (20). Udongo kiasi kidogo utumike katika kufunika mbegu.

Baada ya mbegu kuota ni vizuri kupunguza baadhi ya miche na uwe katika kipimo cha sentimita 2-3 toka mche hadi mche. Hii itasaidia kuwa na miche mifupi na yenye nguvu. Inafaa kunyeshea kitalu mara moja au mbili kwa siku na katika sehemu za joto ni vizuri kuweka kivuli katika matuta. Katika wiki ya tatu, hadi wiki ya nne, ni vyema kuondoa kivuli kidogo kidogo huku ukipunguza unyeshaji. Hali hii itasaidia miche isipate mshtuko wa uhamishaji shambani.

Kuhamisha na kupanda

Hamisha na kupandikiza miche shambani ikiwa na umri wa wiki nne, wakati huo miche ikiwa na majani manne ya mwanzoni na urefu wa kiasi cha sentimita kumi na mbili (12). Wakati wa upandaji, ni vizuri udongo ukashindiliwa kwenye kila mche. Inafaa upandaji ufanyike mara moja, na ni vizuri ukafanyika nyakati za jioni au asubuhi sana, na udongo uwe na unyevu wakati wote.

Nafasi kati ya mmea

Katika mstari hadi mstari inatakiwa iwe sentimita 60-75. Kutoka mmea hadi mmea ni sentimita 30-60. Pia sentimita 75-90 inaweza kutumika kati ya mstari na mstari.

Mbolea: Ni vizuri kuweka kiasi cha viganja 2-3 vya mbolea ya samadi iliyooza vizuri katika kila shimo.

Palizi: Wakati wa palizi ni vizuri mkulima akawa mwangalifu ili asiharibu mizizi. Wakati kabichi inapoanza kufunga hufunika ardhi, hivyo, husaidia kuzuia magugu yasiote, kwa wakati huu hakuna haja ya kupalilia.

Kuvuna: Kabichi hukomaa katika kipindi cha siku 60-100 tangu kupandwa. Kwa ajili ya kuuza ni vizuri kuvuna wakati vichwa vinapofunga vizuri na huwa na uzito wa kutosha kabichi iangaliwe na kutunzwa baada ya kuvunwa ili isikwaruzwe na kuoza kabla ya kutumiwa. Kwa kawaida hekta moja hutoa mavuno kiasi chatani 50-80.

Aina za kabichi
Kuna aina nyingi za kabichi na zifuatazo ni miongoni mwa aina hizo:
Cabbage Jersey
Early Jersey wakefield – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
Cabbage Sugar loaf
Sugar loaf – Aina hii hukomaa mapema sana, kiasi cha miezi 2.5
Cabbage Gloria
Glory of enkhuizen – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
Prize drumhead Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
Prize drumhead – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3.5
F1-High Breed Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4
F1-High Breed – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 2-4
Cabbage Duncan
Duncan – Aina hii hukomaa katika kipindi cha miezi 3


** Majina hayo yanabaki kama yalivyo kutokana na sheria za hati miliki ya watafiti.

Ufugaji Ng'ombe: Mipango thabiti huleta mafanikio katika ufugaji


Mipango thabiti huleta mafanikio katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Wafugaji waliofanikiwa wanafahamu fika kuwa katika uzalishaji wa maziwa 20% inatokana na aina ya ng’ombe na 80% matunzo.

Tumekutana na kupokea maombi kutoka kwa watu wengi ambao wanataka kuanzisha ufugaji wa ng’ombe, lakini hawajui ni wapi pa kuanzia. Kwa kawaida, wao wanaweka pesa, kutafuta ng’ombe, kununua na mwisho hupata ng’ombe. Hapo ndipo kuhangaika na kupata msongo wa mawazo kwa mfugaji huanza kwa kuwa ng’ombe hazalishi maziwa kutokana na aina yake pekee.

Kwa wafugaji wadogo walio wengi, wakati ambapo ng’ombe anafika zizini kwake wanakuwa bado hawajawa tayari kumpokea ng’ombe huyo kwa ajili ya ufugaji. Ili ujasiria mali kwa njia ya ng’ombe uweze kufanikiwa na kumfaidisha mfugaji kiuchumi, mfugaji ni lazima ahakikishe kuwa miundo mbinu muhimu inakuwa tayari kabla ya kumleta ng’ombe.

Kwa mujibu wa mwongozi wa kitabu cha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa Afrika ya mashariki, ng’ombe wa maziwa ni lazima wapate mahitaji yafuatayo:
• Malisho bora na maji safi ya kunywa
• Afya bora bila majeraha
• Mazingira safi ikiwa ni pamoja na  banda lililojengwa vizuri
• Uangalizi mzuri na wa kirafiki,  ambao humfanya ng’ombe kuwa mtulivu bila kuwa na msongo.

Bila mahitaji haya muhimu, na mfugaji kutokumtunza ng’ombe vizuri, asitegemee kuwa ng’ombe huyo atazalisha kiwango kizuri cha maziwa. Uzalishaji wa kiwango cha maziwa na ubora wake unategemeana kwa kiasi kikubwa na mambo hayo yaliyotajwa hapo juu. Wataalamu wanasema kuwa 20% ya uzalishaji wa ng’ombe inatokana na aina ya ng’ombe na 80% matunzo kutoka kwa mfugaji. Muhudumie ng’ombe wako vizuri naye atarudisha kwa kuzalisha maziwa vizuri.

Mipango

Wafugaji ni lazima wawe na mipango thabiti kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe. Hii hujumuisha idadi ya ng’ombe mfugaji anayotaka kufuga, pamoja na kufahamu ni kiasi gani cha malisho kinachohitajika kwa kipindi chote cha mwaka. Mfugaji pia anapaswa kufahamu kuwa ni kwa namna gani malisho yanafaa kutolewa kwa wanyama.

Mfugaji ni lazima pia apange ni kwa namna gani atapata malisho kwa kipindi chote. Hii inamaanisha kuwa ni muda gani atapanda, kuvuna na kuhifadhi. Mipango ni nguzo muhimu sana kwa kuwa inawezesha kusaidia kufahamu ni nini cha kufanya, namna ya kufikia malengo yaliyokusudiwa, na ni hatua gani imefikiwa. Mfugaji ambaye hana mipango thabiti ni sawa na mtu anayeanza safari bila kufahamu mwisho wa safari yake ni wapi.

Mahitaji ya mlo kamili

Shughuli ya ufugaji wako itakamalika siku ambayo utaweza kuelewa uhusiano kati ya ulishaji wa ng’ombe, uzalishaji wa maziwa na mapato. Endapo ng’ombe wa maziwa atalishwa kwa malisho hafifu ni dhahiri kuwa uzalishaji wa maziwa pia utakuwa hafifu.

Malisho bora

Tafuta ni aina gani ya malisho hufanya vizuri katika ukanda wako. Malisho endelevu hutegemeana kwa kiasi kikubwa na aina ya malisho na utunzaji wake shambani mwako. Chukulia kuwa wewe ni mfugaji mdogo na hauwezi kumudu gharama za umwagiliaji, ni lazima utumie kwa kiasi kikubwa malisho ya wakati wa mvua na kuhifadhi ili kuweza kuyatumia wakati wa kiangazi.

Inashauriwa kupanda majani ya malisho kwa kiasi kikubwa uwezavyo wakati wa mvua. Wahamasishe majirani zako kupanda malisho pia, ili baadaye uweze kununua kutoka kwao. Matete, nyasi, majani ya mtama, majani ya mahindi, lusina, desmodiamu, na alizeti ni miongoni mwa malisho ambayo hufanya vizuri katika maeneo mengi nchini Tanzania.

Kiwango cha kutosha

Fahamu ni kiwango gani kinachotosha kwa kila ng’ombe wako. Hii itakusaidia kufahamu ni kiasi gani cha malisho upande na ni kiasi gani uhifadhi. Kwa wastani, ngombe wa maziwa aliyekomaa mwenye uzito wa kilo 400, anayefugwa ndani ana uwezo wa kula kilo 12 za majani makavu kwa siku. Kumbuka kuwa endapo mifugo yako haitapata malisho ya kutosha wataonesha kwa muonekana wao, na kisha kukupa adhabu kwa kuzalisha maziwa kidogo sana. Kama kanuni inavyoeleza, hakikisha kuwa 15%-18% ya malisho yote ni protini.

Zingatia utunzaji na uzalishaji wa malisho vizuri

Wafugaji walio wengi hukwepa kupanda majani ya malisho kwa kuogopa gharama ya mbolea na mbegu. Kwa uzoefu wetu mfugaji anaweza kutumia mbolea inayotokana na wanyama kupanda malisho na kuyatunza vizuri. Matete ni moja wapo ya malisho hayo. Endapo malisho hayo yatawekwa mbolea vizuri, shamba dogo tu la malisho linaweza kukupatia malisho ya mifugo kwa kipindi chote cha mwaka.

Weka malisho katika hali ya usafi

Hifadhi malisho katika sehemu nzuri, sehemu ambayo hayatapigwa na jua moja kwa moja, mvua au kuwepo uwezekano wa vitu vingine vinavyoweza kuyaharibu kama vile siafu na wadudu wengineo. Majani ya malisho ni lazima yanyaushwe vizuri kuepuka viini vya sumu vinavyoweza kuwepo kwenye malisho. Mfugaji anaweza kuamua juu ya ubora wa malisho kutokana na muonekano wake, harufu na mguso. Malisho mabichi yenye wingi wa majani kuliko shina, yenye kijani kilichokolea, na ambayo yana mguso nyororo, ni moja ya malisho bora ukilinganisha na yale yenye ugumu, shina kubwa na rangi ya njano. Epuka kulisha mifugo yako kwa kutumia malisho yenye ukungu kwa kuwa yanaweza kuwa na sumu.

Kuweka kumbukumbu ni muhimu

Uwekaji wa kumbukumbu ni muhimu lakini huwa hauzingatiwi na wafugaji walio wengi. Baadhi ya wafugaji huona kama uwekaji wa kumbukumbu ni kazi ya ziada, ambayo kulingana na wao haina uhusiano wowote na mapato yanayotokana na shughuli zao. Hata hivyo, bila uwekaji sahihi wa kumbukumbu, mfugaji hawezi kufahamu ni mapato kiasi gani anayopata kutokana na shughuli ya ufugaji. Ni kwa namna gani mfugaji anaweza kufahamu wakati wa kumpandisha ng’ombe wake, kama hajui kuwa zimepita siku ngapi tangu ng’ombe huyo alipozaa!

Alizeti ni chanzo cha malisho ya mifugo


Alizeti haitoi mailisho pekee, pia inatoa mafuta bora kwa afya ya binadamu na pia malighafi inayotumiwa na nyuki kutengeneza asali.
Unapotengeneza chakula cha mifugo peke yako, si tu kupunguza gharama, lakini pia inakupa uhakika wa kuwa na chakula bora. Pia Wafugaji wa nyuki wanaopanda alizeti wanapata faida ya ziada kwa kupata asali iliyo bora kwa sababu nyuki hukusanya poleni kutoka kwenye alizeti wanapofanya ushavushaji.

Chanzo kizuri cha protini

Chakula cha mifugo kinachotengenezwa kutokana na alizeti ni chanzo kizuri cha protini kwa ajili ya mifugo, hasa ng’ombe wa maziwa, kuku, nguruwe na hata sungura. Malisho haya yana kiasi kikubwa cha protini, nyuzi nyuzi na kiasi kikubwa cha mafuta. Malisho haya yana protini kiasi cha asilimia 29-30, kiasi cha nyuzi nyuzi asilimia 27-31.

Moja ya tabia nzuri ya alizeti ni kwamba haina vitu vinavyoathiri virutubisho kwa mifugo, hata hivyo, ina kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi na mashudu yake kuwa magumu kiasi, jambo ambalo husababisha ugumu kidogo kwenye kusagwa tumboni. Mbali na virutubisho vya aina nyingine, alizeti ni chanzo kizuri cha kalishamu, fosiforasi na vitamini B.

Ubora wa alizeti inayotumika kwa ajili ya malisho ya mifugo inategemeana na namna ambayo imetayarishwa. Kwa mfano, alizeti inayosagwa bila kuondoa maganda ya nje, ina kiasi kikubwa cha nyuzi nyuzi (kati ya asilimia 27-30, lakini inakuwa na kiasi kidogo cha protini asilimia 23). Alizeti ambayo imetayarishwa kwa ubora wa hali ya juu huwa maganda yameondolewa na inakuwa na kiasi kikubwa cha protini, kiasi cha asilimia 40.

Mkulima anapaswa kufahamu kuwa alizeti bado inakuwa na virutubisho hata kama haitatayarishwa kwa ustadi. Mfugaji anaweza kutumia soya na karanga badala ya alizeti, lakini ni lazima apeleke alizeti kupima kuhakikisha kuwa ina nyuzinyuzi na virutubisho kwa kiwango cha nyuzinyuzi na protini kinachokubalika.

Inapendekezwa kutumia alizeti

Kulingana na utafiti ambao umefanyika nchini Tanzania, alizeti iliyochanganywa na pumba ya mahindi kwa kiasi cha asilimia 30, kisha kulishwa ng’ombe aina ya Zebu ina uwezo wa kuongeza uzalishaji wa maziwa kutoka lita 6.6 kwa siku mpaka lita 8.1 kwa siku. Nchini Zimbabwe, mashudu ya alizetu huchanganywa na mahindi pamoja na  mabua ya mahindi ambayo yamewekwa urea kwa kiwango cha wastani wa kilo 4.4 kwa siku, na kulishwa ng’ombe aina ya Jersey pamoja na ng’ombe chotara ambao hulishwa katika machungo ya wazi, Ng’ombe hawa huongeza kiasi cha maziwa kwa wastani wa kilo 5.8 mpaka kilo 6 kwa siku.

Aina ya alizeti

Kuna aina mbili za alizeti, alizeti fupi na alizeti ndefu. Aina ndefu hurefuka mpaka kufikia kiasi cha urefu wa mita 1.5-2.4. Uzalishaji wake ni hafifu ukilinganisha na mbegu za kisasa. Aina hii mara nyingi huwa ile inayojulikana kama Hungary nyeupe na Fedha. Alizeti fupi ni inayotokana na mbegu za kisasa ambayo huwa na urefu wa mita 1.2, aina hii huwa na mavuno mazuri zaidi ukilinganisha na aina ndefu.

Kutengeneza chakula cha mifugo

Kilo tatu na nusu za alizeti inapokamuliwa hutoa mafuta lita moja na mashudu kilo mbili na nusu.

Resheni kwa ng’ombe wa maziwa

•Changanya kilo 18 za mashudu ya alizeti na kilo 100 za pumba ya mahindi ili kutengeneza chakula cha ng’ombe.
•Mlishe ng’ombe anaezalisha maziwa kwa wingi kiasi cha kilo 4 ya mchanganyiko huo na kilo 2 kwa ng’ombe anaezalisha kiasi kidogo cha maziwa.
•Mbali na kulisha mchanganyiko huo, ng’ombe wa maziwa ni lazima apewe kiasi kingine cha chakula cha kawaida cha kila siku kama vile matete, hay, au aina nyingine yoyote ya malisho bora kwa kiasi cha kutosha.

Resheni kwa ajili ya kuku

Chakula cha kuanzia: Changanya kilo 22 za mashudu ya alizeti na kilo 100 za pumba ya mahindi Chakula cha kukuzia: Changanya kilo 20 za mashudu ya alizeti na kilo 100 za pumba ya mahindi au chenga.
Chakula kwa ajili ya kuku wanaotaga: Changanya kilo 18 za mashudu ya alizeti na kilo 100 za chenga za mahindi

ZINGATIA: Unapotengeneza chakula kwa ajili ya ng’ombe wa maziwa, mfugaji ni lazima ahakikishe kuwa mashudu hayazidi asilimia 20 ya resheni ya kulishia. Kwa ajili ya kulishia kuku, alizeti isizidi asilimia 7 ya jumla ya resheni.

Namna ya kuzalisha alizeti

Hali ya hewa: Alizeti hustawi vizuri zaidi kwenye udongo tifutifu, wenye rutuba ya kutosha. Zao hili lina mizizi inayoenda chini kwa kiwango cha kikubwa hivyo kuiwezesha kustawi hata katika sehemu yenye kiwango kidogo cha mvua. Kiasi cha wastani wa milimita 500-750 za mvua zinatosha kabisa kwa uzalishaji wa alizeti. Inaweza kulimwa kutoka usawa wabahari mpaka kufikia mwinuko wa mita 2600 kutoka usawa wa bahari.

Maandalizi ya shamba

Ni lazima kuhakikisha kuwa shamba limelimwa vizuri, ili kuweza kupata sehemu nzuri ya kusia mbegu.
Nafasi: Mbegu zinaweza kupandwa kwa nafasi ya sentimita 75 kwa 30 kwa kiasi cha kilo 2 kwa ekari moja (sawa na kilo 5 kwa hekari). Panda mbegu 3 kwa kila shimo, kisha acha mmea mmoja kwa kila shimo mimea inapofikia urefu wa sentimita 10-20.

Matumizi ya Mbolea

Alizeti hufanya vizuri kwenye udongo wenye rutuba. Matumizi ya mbolea inayotokana na miamba aina ya fosifeti inafaa zaidi kwa kuwa alizeti inahitaji fosifeti kwa kiasi kikubwa. Matumizi ya mbolea mboji iliyoandaliwa vizuri itaongeza virutubisho vya ziada kwenye udongo.
Alizeti hukua vizuri katika sehemu isiyokuwa na magugu. Palilia alizeti inapokuwa na urefu wa mita 0.7 (Kiasi cha wiki 4).

Ndege waharibifu

Ndege wanaweza kuharibu kiasi cha asilimia 50 ya alizeti endapo hawatafukuzwa. Ili kuzuia uharibifu huo, mkulima anaweza kuchukua hatua zifuatazo;
•Vunja shina la alizeti kufikia usawa wa magoti kabla ya alizeti kukauka. Unaweza pia kuvunja katika urefu wowote lakini alizeti iangalie chini ili kuzui ndege kudonoa.
• Ondoa alizeti shambani baada ya kukauka na kuihifadhi.
• Ubanguaji unaweza kufanyikia nyumbani kwa kutumia fimbo
• Alizeti ni lazima ikaushwe mpaka kufikia kiwango cha unyevu wa asilimia 10 kabla ya kuhifadhiwa

ASIA MORGAN ADAI TALAKA


MREMBO ambaye aliwahi kunyakuwa Taji la Unique Model, Asia Morgan ambaye pia ni msanii wa filamu anayechipukia, amefunguka kuwa endapo mwigizaji Slim Omary aliyekuwa mumewe hatampa talaka, atampa yeye


Msanii wa filamu Bongo anayechipukia, Asia Morgan.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Asia ambaye alitengana na Slim akimtuhumu kuwa na wivu wa kupindukia, alisema licha ya kudai talaka mahakamani Slim amekuwa mzito kuitoa hivyo dawa yake ni yeye kumpa.

“Unajua mimi na Slim tusingeachana kwa malumbano kiasi hiki yeye ndiyo chanzo sasa kwa kuwa anagoma kuniandikia takala yangu, nitamuandikia yeye ili tuondoe mzizi wa fitna,” alisema Asia.

Ted Cruz Suspends His Campaign for President

Video
INDIANAPOLIS — Less than a month ago, Senator Ted Cruz seemed to have done it.
He had won Wisconsin. Former rivals were holding their noses to support him. He was dominating delegate elections, positioning himself for what seemed increasingly likely to be a floor fight at the Republican convention in July, as the campaign of Donald J. Trump fell into internal disarray.
“Tonight is a turning point,” Mr. Cruz said on primary night in Milwaukee. “It is a rallying cry.”
It was neither.
On Tuesday, Mr. Cruz ended his campaign, his loss in Indiana extinguishing any chance of denying Mr. Trump the nomination.
“Together we left it all on the field in Indiana,” Mr. Cruz told supporters here as cries of “Nooo!” rained from the crowd. “We gave it everything we’ve got. But the voters chose another path.”
Yet to dismiss Mr. Cruz as an also-ran would diminish his unlikely feat in outlasting nearly every rival: His calls for conservative purity were, for better or worse, the most consistent message in the field, his rage against the “Washington cartel” a signal of the nation’s ever-dimming view of its leaders.
In a year when many voters flocked to the candidate they hoped could startle Washington into submission, Mr. Cruz galvanized millions of supporters drawn to his more ideological conservatism, quoting founding documents and free-market texts. He was the most right-leaning candidate to even sniff the nomination in at least a half-century.
Long before Mr. Trump careered into the race, Mr. Cruz staked perhaps the loudest claim to the boiling national anger among hard-line conservatives in the age of President Obama.

For a candidate who appeared, just a few weeks ago, to have a plausible path to the nomination, the descent came quickly. The calendar did not help.
Hours after his Wisconsin victory, he charged headlong into New York City, earning Bronx jeers that foretold a hostile reception across a half-dozen Eastern states that were never a natural fit for him.
“Manhattan has spoken!” Mr. Cruz joked bitterly in Indiana. “Everyone give up and go home.”
But the problems ran deeper.
Given an opening to unite the party in opposition to a man many see as an existential threat to it, Mr. Cruz was unable to consolidate support, leaving Republican leaders lurching toward a fateful bet: Live with the risk of a Trump nomination rather than elevate a figure they loathe.
His advisers insisted that he was a more versatile candidate than past Iowa caucus winners like Mike Huckabee and Rick Santorum, but he failed to sufficiently expand his appeal much beyond the party’s most religious and ideological voters. His surrogates in Indiana looked much the same as in Iowa, with faith-inflected testimonials from the radio host Glenn Beck and Representative Louie Gohmert of Texas.
“Conservatives are uniting,” Mr. Cruz said often on the campaign trail, long after it felt true. But his efforts were undercut, in large measure, by his toxic relationships with Senate colleagues and a manifest indifference to repairing them.
Soon, the indignities mounted. He named Carly Fiorina his prospective running mate, despite trailing by several hundred delegates, briefly rousing a partly full Indianapolis pavilion.
“Sir, with all respect,” Mr. Cruz pleaded, after approaching one of them for a chat on Monday, “Donald Trump is deceiving you. He is playing you for a chump.”
On Tuesday morning, he at last unburdened himself in full, promising to tell reporters “what I really think of Donald Trump” for the first time.
“This man is a pathological liar,” Mr. Cruz said, ticking off Mr. Trump’s distortions, his infidelities, his penchant for conspiracy theories. “The man is utterly amoral.”
It is possible there is nothing more Mr. Cruz could have done.
Mr. Trump has proved immune to political gravity. He has been largely impervious to attacks, once Mr. Cruz backed away from his monthslong embrace and began hammering him.
Most critically, Mr. Trump’s success in early states across the South, thought to be Mr. Cruz’s firewall, forced a rewrite of the Cruz campaign playbook on the fly.
But while few politicians have better absorbed the lessons of the party’s rightward tilt in recent years, Mr. Cruz found himself outmaneuvered on issues like trade and national defense by an outsider whose political antenna had a crisper signal.
Even on immigration — where Mr. Cruz’s grasp of the party’s id helped vanquish a foe, Marco Rubio, who came to regret embracing a pathway to citizenship — Mr. Trump managed to go bigger and louder.
 
 
 
That Mr. Cruz lasted this long anyway was a triumph of management guile and considerable hustle: No Republican campaign more effectively marshaled its finances, holding the most cash on hand for much of the race, and no candidate worked harder than he did, frequently dashing through six events a day in Iowa.
With a showman’s itch and a singular manner of speaking — the long pauses, the controlled twang, the easy deployment of words like “élan” and “hosannas” on the stump — Mr. Cruz registered at times like an actor playing the role of presidential candidate.
He often resorted to gimmickry, from re-enacted movie scenes to lawyerly theatrics to his grandest stunt of all: adding Mrs. Fiorina to an imagined ticket.
But these last few, flailing weeks belied a campaign that for months had followed its initial strategy to the letter.

Mr. Cruz and his advisers often likened the election to a college basketball tournament bracket, where opponents like Scott Walker and Mr. Rubio were to be muscled out one by one. (They also griped that Gov. John Kasich of Ohio failed to leave the court, despite the score.)
When Mr. Cruz entered the race, his team openly cheered its meager position, roughly 5 percent in the polls, reasoning that he could energize his core supporters first.
“You have to own a base in the Republican primary,” his campaign manager, Jeff Roe, said the day Mr. Cruz announced his run at an evangelical university last year. “If you own the base, then you can grow it.”
Mr. Cruz’s most consequential choice might have come last year when he defended Mr. Trump as a credible outsider and a force for good in the race as rivals began taking swings.

As late as December, he celebrated Mr. Trump as “terrific,” rising quietly in the polls as Mr. Trump absorbed the slings and arrows directed to a front-runner.
Even after Mr. Trump began disparaging Mr. Cruz’s Canadian birth, the senator initially resisted a full-scale barrage. Eventually, his broadsides were frequent and scattershot: Mr. Trump was too unsteady, too shifty, too consumed by social media, too much like Hillary Clinton.
Recently, as Mr. Cruz’s growth seemed to reach its outer bounds, he leaned increasingly on this sort of messaging potpourri.
He tried positioning himself as the party’s champion of women. He cast himself as the heir to President Obama’s generational promise, debuting a new slogan — “Yes, we will!” — that was quickly abandoned.
Then there was his habit of declaring as fact things he wished to be true. Mr. Cruz often described the “hard ceiling” of support that Mr. Trump would surely brush up against, estimating it to be 35 to 40 percent.
“Donald has been a minority candidate, a fringe candidate,” Mr. Cruz told reporters last week.
The next day, Mr. Trump received at least 54 percent of the vote in all five primaries.
And if Mr. Trump’s chosen moniker for Mr. Cruz (“Lyin’ Ted”) was not quite as instantly devastating as some of his others (“Low-Energy” Jeb Bush, “Little Marco” Rubio), the Cruz campaign contributed to lending it a ring of truth — not least because of his abrupt antagonism toward Mr. Trump after reams of praise.
While Mr. Cruz steadied himself, rebounding in his home state of Texas and winning several smaller contests and delegate conventions, his successes were too few.
Even in victory, Mr. Cruz spoke often in apocalyptic terms. Facing defeat, his pleas grew pained.
“If Indiana does not act,” he said hours before Tuesday’s vote, “this country could well plunge into the abyss.”

George Clooney and his wife Amal checked into one of the new hotels on Zanzibar.


Dreaming away the day on Zanzibar: Coral reefs, colonial history and chic cuisine on Tanzania's grand slice of ocean paradise

  • Pitched 25 miles east of Tanzania, Zanzibar is an Indian Ocean haven
  • The island is rich in cultural heritage from both the Omani and British eras
  • It has a reputation for backpacker tourism - but also has luxury enclaves 
  • A-list couple Amal and George Clooney stayed on the island last summer 


George Clooney and his wife Amal checked into one of the new hotels on Zanzibar last summer - a boutique retreat hidden down a sandy path leading to an indigo ocean.
This celebrity endorsement is significant. It confers on an island where sultans once ruled a kind of Papal blessing; a dash of A-list stardust.
Until a few years ago, Tanzania's feted Indian Ocean island was largely seen as a destination for backpackers, albeit one with an intriguing history as an outpost of British colonial rule. David Livingstone used it as a base in his search for the source of the Nile.
A blue-sky portion of paradise: Zanzibar offers beaches where the beauty of the scenery is astounding
A blue-sky portion of paradise: Zanzibar offers beaches where the beauty of the scenery is astounding
I have neither the great explorer's wanderlust, nor the Hollywood actor's star quality - but I, too, am lured by Zanizbar's reputation for being untouched.
Rising at daybreak to walk along a deserted beach to the northerly fishing village of Nungwi, I watch fishermen still at work, hauling in a night catch of slippery, silver tuna and marlin: air still in their gills, nets around their fins.
As the sun climbs, the fishermen shelter under palm trees to mend their nets. Women arrive at low tide, wearing brightly coloured kangas — kimono-like wraps — to collect seaweed to be made into creams. There are no jet-skis or kite-surfers.
Zanzibar is located 25 miles off the coast of Tanzania and six degrees south of the Equator. But it basks in a comfortable average year-round temperature of 28C. It is ringed by coral reefs and talc-soft sand that separates coconut forests from the sea.

FIKIA NDOTO ZAKO






Je unajiuliza uanze wapi ili kufikia ndoto zako za maisha ya kimataifa iwe kufanya kazi nje ya nchi, au kuwa na ushirikiano na watu wa mataifa mbalimbali. Katika makala hii naeleza mambo ya msingi ya kuzingatia ili uweze kuwa mshirika wa jumuiya ya kimataifa yaani uweze kuwa na marafiki na washirika toka mataifa mbalimbali katika shughuli zako halali za kila siku.  Mambo haya ninayoeleza ni kwa uzoefu wangu na kujifunza toka kwa watu wengine, kitu tunachoita international exposure, yaani uzoefu wa kimataifa kwa kutembea na kuishi nchi tofauti tofauti.

Tamaduni za kuacha:
Kuna mambo kadhaa umejizoesha kuyafanya na ingawa twajua wazi si sahihi na yanakera wengine bado tunaendelea kuyafanya kwa kisingizio tuu eti hivyo ndivyo tulivyo. Ninasema twajua yanakera kwakuwa sisi tukifanyiwa mambo hayo hayo yanatukera. Mfano endapo utamuambia mtu utafanya kitu fulani, kisha usifanye kwa sababu fulani pengine ya kusahau au kutotilia maanani, wajua wazi kua hata wewe usingependa kutegemea jambo toka kwa mtu halafu mtu huyo asikufanyie.
Katika maisha ya kimataifa , ustaarabu ni kuthamini muda wa wengine, ni kuwajali wengine na kufanya mambo unayoahidi utafanya. Na kama hautoweza kufanya, basi utoe taarifa kwa wakati muafaka kuwa hautoweza.
Kuwa muwazi, mkweli na kuwajibika katika jukumu unalotarajiwa kufanya ni mambo yanayotarajiwa kutoka kwako ili uweze kufiti kuishi na watu wa mataifa tofauti wenye kuweza kushirikiana nawe kufika mbali kimaisha.

Uwezo wa kufikiri kwa akili ya kawaida na kubadilika
Kuna mambo mengi tunaamini na kufuata bila kufikiria sisi wenyewe. Pengine unafuata na kuamini mambo fulani sababu tuu ulisoma hivyo darasani, watu wengi wanaamini hivyo basi itakuwa ni sahihi, au kwakuwa watu fulani wenye vyeo, watu maarufu wa wakubwa kwako ki umri wanasema hivyo. Uwezo wako kuwa salama na kufanikiwa katika maisha ya kimataifa unahitaji sana uwezo wako binafsi wa kufikiri na kufanya maamuzi kwa kupima maelezo kwa akili yako ya kawaida tuu (common sense).
Utakutana na watu wengi wenye malengo tofauti hivyo utapata mitazamo na taarifa tofauti. Hautotakiwa kuamini zote, utatakiwa kuchuja wewe mwenyewe na kufanya maamuzi yenye manufaa kwako. Jifunze sasa kuhoji mambo, chunguza maamuzi yako na ujihoji hadi wewe mwenyewe . Tafuta taarifa zaidi ya unayoamini kuwa ni ukweli, unayosikia, na ukubali kuwa tayari kubadilika kimtazamo endapo utakuta kuwa ulichokuwa ukidhani ni sahihi sikuzote kumbe sio.
Uwezo wa kufanya mawasiliano

Nimeongelea sana umuhimu wa kujua kufanya mawasiliano kwa ufasaha na namna ya kufanya mawasiliano katika makala FANYA HIVI KAMA UNATAKA KUPATA UFADHILI WA MASOMO AU MTAJI WA BIASHARA.
Ujuzi wa lugha
Pointi hii haihitaji maelezo kufafanuliwa sana kwani bila ujuzi wa lugha ya mawasiliano, hakuna kitu utaweza kufanya katika ulimwengu wa kimataifa, haijalishi uwezo wako wa kielimu, au bidii zako kikazi. Fahamu lugha kuu ya mawasiliano yaani Kiingereza.

Umuhimu wa ndoto
Ninaposema ndoto ninamanisha uwezo wako wa kufikiria na kutumaini mambo makubwa, sio ndoto zile za usingizini.  Uwepo wa ndoto unakufanya utengeneze mwelekeo wa namna gani maisha yako unatakiwa uyaendeshe sasa ili kufikia huko unapotaka kuenda. Mfano kama unaota kuwa siku moja uende kufanya kazi nje ya nchi, basi bila shaka utaanza sasa kujifikiria namna gani ya kujiimarisha katika lugha ya kigeni na pia kuanza juhudi za kupata taarifa zaidi kuhusu maisha nje ya bongo. Usipokua na ndoto, basi utajichukulia poa na hivyo kutofanya juhudi sana.

Kuwa karibu na mtandao (Internet)
Matumizi ya mtandao ni zaidi ya kutumia Facebook , Instagrams, Blogs na WhatsApp.  Baadhi ya watu huishia kutumia simu zao kwa ajili ya mitandao ya kijamii, na wakizidi sana watatumia Google kutafuta taarifa fulani.  Maisha ya kimataifa yanakuhitaji uwe na uzoefu na taarifa tofauti tofauti nyingi kuhusu mataifa –siasa , uchumi, tamaduni, teknolojia na matukio makubwa. Na zaidi sana uwe na taarifa sahihi au zinatoka kwa vyombo huru na vya kuaminika na sio toka kwa watu wanao copy na kupaste kwa blogs zao au kwa akaunti zao za FB bila kufanya utafiti.
Kuwa na taarifa sahihi na kuzashare kunakufanya uaminike na kuonekana mtu sahihi wa kushirikiana katika mazungumzo.
Pia jizoeshe kutumia email kwa mawasiliano na mara kwa mara ufungue na kutumia akaunti yako ya email.

MWONGOZO KWA MJASIRIAMALI


MAANA YA UJASIRIAMALI
       Ujasiriamali ni hali ya kutumia     mbinu mpya za kiubunifu na ujuzi     katika utoaji  wa huduma/ biashara.
       Ni hali ya kuweza kutambua fursa zilizokuzunguka ili kufikia ndoto zako kwa kutumia ubunifu
       Mjasiriamali       ni mtu ambaye hutumia mbinu mpya na ubunifu , ujuzi na maarifa katika utoaji wa huduma
       Mjasiriamali ni mtu anayetaka mabadiliko katika maisha kutoka hapo alipo na kuboresha maisha akiwa na ujasiri wa kufikia malengo yake kwa kuthubutu. 
 
       SIFA ZA MJASIRIAMALI
             Ã Ni mbunifu
             Ã Ni mdadisi wa mambo
             Ã Anashauhuku ya kujifunza
                 kutoka kwa waliofanikiwa
            Ã Ni mvumbuzi katika utendaji
            Ã Anathubutu katika kufanya
                mambo(Sio mwoga).
 
JINSI YA KUBUNI WAZO ENDELEVU LA BIASHARA
       Wazo la biashara ni maelezo mafupi yahusuyo biashara au shughuli unayotaka kufanya.Kwa mfano kushona nguo,kulima bustani, kufuga kuku, kuuza chakula   cha mifugo n.k.
       Wazo la biashara linahusu:
     n Nini unachotaka kufanya kumridhisha 
          mteja/kukidhi kiu yake.
      nNi huduma gani/bidhaa unayotaka kuuza 
          sokoni.
      nWateja wako ni wa aina gani?
       nJinsi ya kutoa huduma/biashara yako 
 
                     
     UMAFUTI  (SWOT ANALYSIS)
 
       Ni kifupisho katika uchambuzi wa wazo endelevu la biashara.
             U- Uwezo Ni pamoja na kuwa na ujuzi, uzoefu na maarifa kwa biashara
              unayotaka kuifanya/kuwa na uwezo wa kutoa huduma /biashara unayotaka
              kuifanya.
MA-  madhaifu
         Upungufu ulionao ambao unaweza kuwa changamoto kwa biashara unayotaka kuifanya
       Kwa mfano mtaji mdogo, kodi ya pango iko juu.
FU-fursa
       Hali na mazingira rafiki kwa biashara /huduma unayotaka kuitoa. Kwa mfano hakuna mtu anayetoa huduma kama unayotaka kuitoa, bei ni rahisi kwa walio wengi, sehemu ya biashara ina muingiliano wa watu mbalimbali
T- tishio
          Vizingiti katika   ufanyaji biasha  unayotaka kuifanya, kwa mfano uwezekano wa watu wengi kufungua biashara kama ya kwako, kubadilika kwa hali ya hewa n.k.
 
JINSI YA KUTANGAZA BIASHARA YAKO
       Kutangaza biashara /huduma yako ni mbinu unazotumia kuhakikisha unavutia wateja . Ni jinsi ya kukidhi kiu ya wateja kwa kuwapa huduma nzuri zaidi ya watu wengine wanaotoa huduma kama ya kwako.
       Mjasiriamali hutumia maarifa, ujuzi na ubunifu ili kuwafanya wateja waende kwake
       Kabla haujaandaa mpango wa masoko kama mjasiriamali ni vyema kufanya utafiti kuhusu huduma unayotaka kuitoa ili uweze kutambua mapungufu na changamoto walizonazo wengine ili uje na  maarifa na mbinu mpya zakuweza kuwavutia wateja wengi zaidi.
 
VITU  4 VYA KUZINGATIA KATIKA MASOKO (BBMK
       B-Bidhaa  ya aina gani unataka kuiweka sokoni na ina utofauti gani na bidhaa za wengine.
       B-Bei ya bidhaa unayotaka kuiweka sokoni.   Katika kupanga bei lazima ujue washindani wako wana gharama gani.
        Kama gharama ziko juu au chini na je, wateja wataweza kumudu, na kama gharama iko juu bidhaa yako umeiongezea ubora gani ili wateja waje kwako na si kwa mwingine.
       M- Mahali unapotaka kuweka biashara yako
        Uchaguzi    mzuri wa eneo la kufanyia shughuli zako ni muhimu kwani ni rahisi kufikiwa na wateja wengi.
       Kama biashara yako haipo karibu na wateja lazima utafute mbinu za kuweza kuwafikia wateja wako  ili waweze kuridhika na kufurahia huduma yako.
       K-Kutangaza bidhaa: Kama mjasiriamali lazima uwe na mbinu mahususi jinsi utakavyofanya bidhaa/huduma yako ijulikane na kuvutia wengi zaidi.Kutangaza ni kuifanya bidhaa yako/huduma iweze kujulikana na mbinu unazozitumia ili mteja aendelee kununua bidhaa/   huduma yako.
 
GHARAMA ZA UENDESHAJI KATIKA UTOAJI HUDUMA
       Katika uendeshaji wa biashara kuna gharama za aina mbili ambazo ni:
       Gharama za moja kwa moja; Hizi ni gharama unazotumia kununua bidhaa unayotaka  kuuza
            Kama vile, mali gafi, nguvu kazi n.k.
       Gharama  ambazo si za moja kwa moja: Hizi ni gharama    nyingine zinazojitokeza wakati wa uendeshaji wa biashara yako, kwa mfano;umeme,ukarabati, bima, riba kwenye mikopo, pango n.k 
 
KUTUNZA KUMBUKUMBU
       Ni muhimu kutunza kumbukumbu katika biashara
       Kutunza kumbukumbu husaidia katika kukokotoa faida au hasara iliyopatikana katika  biashara.
       Hutoa takwimu kuhusu mwelekeo wa biashara na huongeza ufanisi katika usimamizi wa biashara.
       Wakati wa  kulipa kodi utunzaji wa kumbukumbu husaidia kulipa kiwango kinachostahili.
       Kushindwa kutunza kumbukumbu kunaweza kusababisha  kulipa kodi chini ya kiwango kinachohitajika (underpay) au huweza kupunjwa kwa kulipa kodi kubwa zaidi ya kiwango kinachohitajika.(Overpay).
       Kumbukumbu za fedha katika biashara ni muhimu katika mpango wa mauzo na gharama  pamoja na mtiririko wa fedha zinazoingia na zinazotoka (Cash in and Cash out) 
 
       KUMBUKUMBU ZA MAUZO NA GHARAMA
       Hizi ni kumbukumbu ambazo huonyesha mauzo, gharama zilizotumika na faida iliyopatikana
       Ni vizuri kuwa na kumbukumbu za kila siku, wiki, mwezi  na mwaka mzima
       Msingi wa hizi kumbukumbu ni kuwa na mpango wa mauzo na gharama ili kuwa rahisi kufanya tathimini ya maendeleo ya biashara
       Faida kutoka kwenye mauzo tunaipata  kwa kuchukua jumla ya mauzo na kutoa gharama zote zilizotumika
       Kwa mfano kama  umeuza 50,000, kibarua ukamlipa 2000, ushuru3000, bidhaa uliyouza uliinunua 20,000
       Faida=50,000   -  (2000 +3000+20,000)
       Faida=50,000  -25,000= 25,000 
 
MPANGO WA MTIRIRIKO WA FEDHA
       Huu ni mtiririko ambao huonyesha kiasi cha fedha zinazoingia na kutoka katika biashara yako.
       Fedha zinaweza kutoka kwa mfano katika ununuzi wa malighafi, kulipa mkopo, kununua vifaa n.k.
       Fedha zinazotoka husaidia katika kutengeneza faida baadae
       Mtiririko wa fedha huonyesha
      1.Fedha zinazoingia
           a. Kiwango cha fedha  mwanzoni
               mwa mwezi
           b.Fedha  zilizoingia kutokana na mauzo
           c. Fedha zinazoingia kutoka vyanzo vingine
           JUMLA YA FEDHA ZILIZOINGIA  =
      2.Fedha zinazotoka

           a.Kwa kununua malighafi na vifaa vingine
           b. Kwa ajili ya nguvu kazi
           c. Gharama zisizo za moja kwa moja
          d.Kulipia mkopo(marejesho)
          e. Gharama nyingine
                    JUMLA YA FEDHA ZILIZOTOKA  =
 
KIWANGO CHA FEDHA MWISHO WA MWEZI
       Kukokotoa kiwango cha fedha Ulichonacho(baki) =fedha iliyoingia kutoa fedha iliyotoka
       Kiwango cha fedha kilichobaki mwishoni mwa mwezi ndio kianzio kwa mwezi unaoanza